Maafisa wa polisi eneo la Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon wanachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo umepatikana chumbani mwake katika kijiji cha Malakisi kata ya Chesikaki ambapo  dalili za kunywa sumu zikidhihirika.

Naibu chifu wa kata ndogo ya Chesikaki Mourice Wetala amesema alipokea taarifa kuhusu tukio hilo kutoka kwa mzee wa kijiji cha Malakisi ambapo uchunguzi wa awali unaashiria  mwanamume huyo Jacob Kinusu mwenye umri wa miaka arobaini na miwili huenda alikunywa sumu

Iliyopelekea kifo chake.

Aidha Wetala amewahimiza wananchi kutafuta ushauri nasaha ili kutatua changamoto wanazopitia kando na kujitoa uhai, hii ni baada ya kubainika kuwa huenda mwendazake alichukua hatua ya kukatiza maisha yake kutokana na changamoto mbalimbali zinazomkumba.

Maafisa wa polisi eneo la Chesikaki tayari wameanzisha uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tukio hilo huku mwili wa mwendazake ukihifadhiwa katika hifadhi ya wafu  kwenye hospitali ya rufaa mjini Bungoma.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE