Akizungumza kwenye kituo kimoja cha habari humu nnchini jumanne usiku,mwenyekiti wa wanasheria Nelson Havi amesema IEBC inalazimika kuendelea na mipango ya uchaguzi mdogo itakayofanyika machi,Nairobi.Alichangia kuwa kutokuwa na naibu gavana ofisini wakati aliyekuwa gavana Sonko alitolewa mamlakani ilimaanisha hakuna budi ila uchaguzi ufanyike.Wakenya lazima watimize haki yao kama wapiga kura.

Pia alisema kuwa uteuzi wa naibu gavana huanza na huisha na gavana ambaye yuko mamlakani kwahivyo gavana ambaye tayari yuko mamlakani hawezi mteua naibu.

Havi pia alidai kuwa aliyekuwa gavana mike sonko alilengwa na mashtaka ndo atolewe ili kupeana nafasi ya uhamisho wa  pesa  kutoka kwenye kaunti hadi  Nairobi Metropolitan Services(NMS).

Katibu mkuu wa ODM Edward Sifuna alikuwepo pia kwenye jopo hilo na anaelezea kuwa uteuzi wa Kananu ulifanywa kulingana na sheria na aliteuliwa na gavana akiwa mamlakani.Alidai kuwa Gavana Sonko ndiye hakufanya kazi yake kwa umakini.

Story by Lavin Wanzetse

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE