Wanaume wameshauriwa kutumia makundi ya wanaume makanisani kuendeleza umoja wa taifa na kukabili uhasama wa kisiasa ambao unashuhudiwa kwa sasa nchini
 

Ni wito wake padri Antony Tsikalata anayesimamia kikundi cha wanaume wakatoliki jimbo la kakamega na pia paroko wa parokia ya Eregi baada ya mkutano na viongozi wa kikundi hicho mjini kakamega ambapo amesema wengi wa wanasiasa ni wanaume na wanapasa kutumia kanisa kukomesha uhasama

Padri Tsikalata amewataka wanaume kuisaidia serikali kutimiza malengo ya kuinua jamii ikiwemo elimu ya watoto

  Ni usemi uliotiliwa mkazo na mwenyekiti wa kikundi hicho cha wanaume wakatoliki jimbo la kakamega Vitalis Arunga

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE