Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, ameingia makubaliano ya awali ya kuichezea Paris St-Germain mpaka mwaka 2026- na sasa klabu hiyo ya Ufaransa inafanya jitihada ya kufanya makubaliano kama hayo na mshambuliaji wa Kifaransa Kylian Mbappe,22.
Kwingineko ni kwamba Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland anaweza kuigharimu klabu yake kiasi cha pauni milioni 34 zaidi kwasababu wakala wake Mino Raiola na baba Alf-Inge wanahitaji pauni milioni 20 kwa kila kamisheni kama sehemu ya mkataba.
By Samson Nyongesa