Wanafunzi_Shule ya Msingi_BukhaywaWanafunzi_Shule ya Msingi_Bukhaywa

Onyo kali limetolewa kwa walimu kutoka eneobunge la Kabuchai watakaopatikana wakijihusisha na visa vya kimapenzi na wanafunzi wa shule za msingi na upili kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria iwapo watapatikana.

Aikuhutubu baada ya kufungua rasmi maktaba katika shule ya upili ya marafiki ya Busakala mbunge wa Kabuchai majimbo Kalasinga, amewatahadharisha walimu dhidi ya kuhusika kwenye  visa vya kimapenzi na wanafunzi huku akielezea umuhimu wa vijana kujiunga na vyuo vya kiufundi.

Wakati uo huo majimbo  amedokeza kuwa maktaba hiyo itawawezesha wanafunzi kufanya vyema shuleni na kuwashauri kutilia maanani swala la elimu watakapokuwa nyumbani baada ya shule kufungwa.

Mwakilishi wadi ya Kabuchai-Chwele Barasa Mukhongo akiwahimiza wanafunzi kuweka bidii shuleni huku mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Busakala Musa Obura akimpongeza mbunge kwa kufungua rasmi maktaba hiyo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE