Ipo haja kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kuboresha baadhi ya barabara katika eneobunge la Mlima Elgon ili kurahisisha shughuli za usafirishaji wa mazao kutoka shambani hadi kwenye viwanda mbalimbali hii ni baada ya kubainika kuwa baadhi ya barabara hazipitiki hasa wakati huu wa msimu wa mvua.

Afisa mkuu mtendaji wa chama cha Ushirika cha Kimama katika wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon Ben Mulupi amehoji kuwa baadhi ya barabara eneo hilo, zimeharibiwa na mvua inayoshuhudiwa kwa sasa na kupendekeza kukarabatiwa japo ameipongeza serikali ya kaunti ya Bungoma  kwa kuboresha baadhi ya barabara za eneo hilo.

Wakati uo huo Mulupi ameishauri serikali ya kaunti hii kuongeza idadi ya maafisa wa kilimo ili kusaidia kuboresha mbinu za kilimo miongoni mwa wakulima eneo hilo.

Amewahimiza wazazi kutumia vyema fedha wanazopokea kama malipo ya zao la kahawa kwa kutenga kiwango bora kushughulikia karo ya wanao, hasa baada ya kalenda ya masomo kubadilika.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE