Wahudumu wa bodaboda kwenye eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani huku wakiendesha biashara yao

Akizungumza kwenye mkutano uliowaleta pamoja viongozi wa wahudumu wa bodaboda eneo la Butali, kamanda wa polisi kwenye eneo bunge hilo Paul Mwenda Nganadha amewataka wahudumu hao pia kutojihusisha na wanasiasa wasio na msingi wa kuwasaidia kujiendeleza wakati msimu wa kisiasa unakaribia

Naye mwenyekiti wa bodaboda kwenye eneo bunge hilo la Malava Chitunga Museve amewataka viongozi na wahudumu wa bodaboda kufanya kazi kwa pamoja huku Timothy Wanami akichaguliwa kama mwenyekiti wa bodaboda wa Butali-Chegulo

Museve ametahadharisha pia wahudumu hao wa bodaboda kutojihusisha na siasa potovu na badala yake washirikiane na viongozi toka sehemu hizo akiwemo naibu gavana wa kaunti ya Kakamega Philip Kutima kuwasaidia kujiendeleza

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE