Wananchi haswa vijana wa kata ndogo ya Sichirai, kata ya Lurambi kaunti ya Kakamega wametakiwa kutojihusisha na suala ya kisiasa. Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Kituo hiki, naibu wa chifu wa eneo hilo bwana Ernest Mayula Ongayo amewataka wale wanao fanya zoezi la kuandikisha watu kutokusanya vitambulisho na badala yake mtu anapaswa kujipeleka mwenyewe kwa minajili ya kusajiliwa

Aidha, bwana Mayula amewaimiza vijana wa kata ndogo ya Sichirai kutotumiwa vibaya na wanasiasa haswa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa elfu mbili ishirini na mbili

Vile vile naibu chifu huyo amewarai wanasiasa kuendeleza miradi walioahidi kutekeleza na sio kujihusisha na campaign za mapema ikizingatiwa kuwa msimu was campaign rasmi haijawadia na pia kuwaonya kutowatumia vijana kufanya vurugu

 By Mary Owano

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE