Wito umetolewa kwa wahisani, serikali za kaunti na serikali kuu kueka zaidi kwenye wanafunzi wanaosomea taaluma za kadri kama vile madereva kama moja wapo ya kuendeleza ajenda kuu nne za serikali za kupambana na umaskini na kutoa nafasi za ajira kwa vijana hao.


Akizungumza na wanahabari ofisini mwake meneja mkuu kwenye chuo cha mafunzo ya kuendesha maghari na pikipiki cha Budget mjini Bungoma Narshon Muhatia amesema kuwa wengi wa wanafunzi wanaofuzu kutoka vyuo vya kadri kufanya vizuri kwenye soko za ajira hivyo basi amewataka wazazi kutokuwa na dukuduku kuwapeleka wanao kupata mafunzo hayo


Vilevile Muhatia Ametumia Fursa hiyo kuipongeza hazina ya maendeleo ya Kandunyi ya CDF kupitia mjumbe wa Kandunyi Atanasi Wafula Wamunyinyi katika juhudi zake za kuendelea kutoa ufadhili kwa baadhi ya wanafunzi shuleni humo
aidha amesema kuwa hivi maajuzi shirika moja la kibinafsi limejitolea kutoa ufadhili kwa takribani wanafunzi kumi jambo ambalo amelishabikia na kusema kua linatia moyo ikizingatiwa wanafunzi kumi jambo ambalo amelishabikia na kusema kuwa linatia moyo ikizingatiwa kwamba wengi wa wanafunzi wana matamanio ya kujifunza udereva ila wanakosa ufadhili


wakati uo huo meneja huyo ameitumiwa fursa hiyo kuwataadharisha madereva haswaa msimu huu wanafunzi wanapoelekea nyumbani kwa likizo fupi huku akiwakumbusha kuwa wao hubeba maisha ya Abiria


Ikumbukwe kuwa chuo cha Budget ni miongoni mwa vyuo vya kufunza uendeshaji magari na pikipiki vinavyotoa wanafunzi wengi wanaotimu kila mwaka. mwaka huu cho hicho kimesajili zaidi ya wanafunzi mia moja na zaidi


By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE