Mshukiwa Navity Mutindi akamatwa kuhusiana na mauaji ya mtoto, Shantelle, idadi ya waliokamatwa sasa yafikia watu watatu.Mwanamke huyo wa miaka 30 alikamatwa na wapelelezi wa DCI akiwa mafichoni mtaa wa Athi River, kaunti ya Machakos.
Inatuhumiwa huenda mshukiwa alidanganya mtoto huyo kuanguka kwa mtego wa wateka nyara ambao walimuua.


Kuna madai kuwa simu yake ni moja ya zilizotumika na watekaji nyara wale kuitisha malipo ya laki tatu kutoka kwa mama mtoto, Christine Ngina.
Siku ya Alhamisi, mahakama ya Kajiado iliamuru wapelelezi kuzuiliwa kwa siku 10 washukiwa Livingstone Makacha Otengo, 27 , na Francis Mbuthia, 42, ambao walikamatwa siku ya Jumatano ili kumaliza upelelezi.
Iliripotiwa kuwa Otengo ambaye ni mwendeshaji bodaboda mjini Kitengela alikamatwa katika eneo la Orata, Kitengela, akiwa na simu inayoaminika kutumika kuitisha pesa kutoka kwa mamake Shantel.
Mikuhu ambaye alikamatwa mida ya saa tatu usiku siku ya Jumatano anatuhumiwa kutumia kitambulisho chake kuandikisha laini ya Airtel ambayo ilipokea pesa zilizoitishwa.Hakimu Edwin Mulochi aliashiria washukiwa wazuiliwe katika kituo cha polisi cha Kitengela kwa siku 10 ili wapelelezi wamalize kazi yao.
Iliripotiwa kuwa mwili wa Shantel, 8, ambaye alikuwa mwanafunzi wa daraja la pili ulipatikana ukiwa umetupwa maeneo ya Orata, Noonkopir siku ya Jumatatu baada ya marehemu kukosekana nyumbani tangu Jumamosi wiki iliyopita.
Baadae Bi. Ngina alijaribu kutafuta mwanawe bila mafanikio kisha akapokea simu kutoka kwa namba isiyotambulika akiarifiwa kuwa mwanawe alikuwa mikononi mwao.Bi Ngina alisema kuwa mwanamke aliyepiga simu alimuagiza kulipa kiwango cha shilingi 300,000 ikiwa alitaka kumuona mwanawe akiwa hai tena.
By marseline musweda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE