Huenda mji wa Nakuru ukatangazwa kuwa jiji hivi karibuni baada ya maseneta kupitisha hoja ya kuinua hadhi ya mji huo ulio katika eneo la bonde la ufa.Kamati ya ugatuzi ikiongozwa na seneta wa Homabay, Moses Kajwang’ ilipendekeza kuinuliwa kwa hadhi ya Nakuru na kuwasilisha ripoti kwenye seneti siku ya Alhamisi
Lililobaki sasa ni rais Uhuru Kenyatta kuukabidhi mji huo hati ya kuthibitisha hali hiyo.

Serikali ya kaunti ya Nakuru iliwasilisha ombi la kufanya Nakuru mji mwezi wa Novemba mwakani 2020. Kufuatana na hayo, kamati ya ugatuzi imekuwa na vikao 11 kuhadiliana kuhusu ombi hilo.Baada ya vikao hivyo, kamati ya ugatuzi ilithibitisha kuwa mji wa Nakuru ulikuwa umefikisha 350,000 ambayo ni juu ya idadi 250,000 na mapato.
Nakuru itakuwa inaungana na Nairobi, Mombasa na Kisumu kwenye orodha ya jiji za Kenya.


Kamati ya ugatuzi ikiongozwa na seneta wa Homabay, Moses Kajwang’ ilipendekeza kuinuliwa kwa hadhi ya Nakuru na kuwasilisha ripoti kwenye seneti siku ya Alhamisi.Kamati hiyo ilionelea kuwa mji huo ulikuwa umeafikia umehitimu kufanywa mji jambo ambalo lilithibitishwa na maseneta wengine.


Baada ya vikao hivyo, kamati ya ugatuzi ilithibitisha kuwa mji wa Nakuru ulikuwa umefikisha matakwa ya kufanywa mji katika maswala ya idadi ya watu na mapato.Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen alisihi serikali ya kaunti ya Nakuru kuwekeza katika kukuza miundombinu ya mji huo.


“Ni sharti serikali ya kaunti ya Nakuru iwe na idara maalum ya mipango na ujumbe wazi kwa wawekezaji wanaotaka kujenga jijini Nakuru kuwa lazima waje na ubunifu wa kipekee kwa mfano jumba lililo na mchoro wa flamingo unaweza vutia watalii sana” Murkomen alisema kwenye seneti.


Gavana wa kaunti hiyo ameshukuru Mungu kwa kupitisha ombi hilo kupitia mtandao wa Twitter.
Nakuru itakuwa inaungana na Nairobi, Mombasa na Kisumu kwenye orodha ya jiji za Kenya.
By marseline musweda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE