Huku shule zikifunguliwa rasmi kwa muhula wa kwanza wito umetolewa kwa serikali kuziangazia shule za kibinafsi wakati inagawa vitabu vya kusoma kwa wanafunzi almaarufu [text books]
Ni usemi wa mkurugenzi wa shule ya kibinafsi ya Little Friends mjini Bungoma Mourice Wanyonyi huku akikariri kuwa wanafunzi wote wanafaa kuhudumiwa sawa na serikali bila kujali misingi ya shule.
Mgurugenzi huyo aidha amesema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na dhana kuwa wanafunzi wanaosomea shule za kibinafsi wanajiweza kifedha jambo ambalo amesema kuwa halina msingi wowote wa ukweli.
Kulingana na maswala ya wanafunzi wa grade five kurejea shuleni baada ya likizo ndefu nyumbani mgurugenzi huyo ametoa wito kwa walimu kuwa makini na wanafunzi hao ili kuhakikisha kuwa wamerejelea masomo sawa sawa.
Ikumbukwe kuwa swala la wanafunzi wa grade five kukaa nyumbani kwa mda mrefu limesemekana na baadhi ya waalimu kuadhiri pakubwa hali yao ya kimasomo huku baadhi ya waalimu wakifichua kuwa baadhi ya wanafunzi hao huenda hawakua wakijisomea nyumbani.
By Hillary Karungani