Wakazi wa eneo bunge la shinyalu wamehimizwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wao wanarudi shuleni wakati shule zinafunguliwa kwa muhula wao wa kwanza wa mwaka 2021. Mca wa isukha kaskazini, elimina llanziva amewataka wazazi kutafuta njia zote zilizopo kupata ada ya shule kwa watoto wao wanapokuwa wakingojea basari kutoka serikali ya kaunti na serikali ya kitaifa kupitia cdf.

Akiongea wakati wa mazishi ya bwana charles shitote lumasai katika kijiji cha bukhaywa katika kata ndogo ya buyangu, bi lanziva aliwahimiza wazazi kusubiri zaidi kwa ufadhili kutoka kwa serikali ya kaunti kwani mfumo wa ifmis unazuia utoaji wa fedha.

Akisisitiza maneno hayo, naibu chifu wa kata ndogo ya lubao bi sulvey shihafu aliwaonya wazazi kwamba kutakua na msako dhidi ya wanafunzi wote ambao hawaendi kwani wazazi walikuwa wamejificha kwa tuuma kua wanafunzi wamemaliza darasa la 4 au darasa la 8 na wanasubiri kujiunga na daraja 5 na kidato cha kwanza. Bi sulvey aliwashauri wakazi kujiandaa kwa kipindi kigumu cha kiuchumi mwaka ujao kutokana na uchaguzi kwani watu watakuwa wanajishugulisha na kampeni na kusahau kwenda shambani.

By Wycliffe Andabwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE