Wazazi katika lokesheni ndogo ya Ifwetere eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wameshauriwa kuwapeleka wanao shuleni huku shule zikifunguliwa nchini kwa muhula wa kwanza
Ni usemi wake naibu chifu wa lokesheni hiyo Paul Ochami akiwahutubia waomboleza kwenye ibaada ya maombi na mazishi ya mzee Jared Harambee Opala mapema hii leo
Ochami amewashauri wazazi pia kutumia vyema vyuo vya kiufundi vya Chombeli na kile cha Shamberere
Wakati uo huo Ochami amewasihi wakaazi wake kwa wale waliopokea jumbe tatu za kudhibitisha kadi zao za huduma number zipo tayari, kufika afisini mwake ili kuzichukua
Ni hafla iliyohudhuriwa pia na wenyekiti wawili wa mashabiki za radio wakiongozwa na mwenyekiti wa mashabiki wa kituo hiki Nelson Andanje pamoja na mwenyekiti wa mashabiki wa kituo cha radio mambo Alex Chitiavi wakiwashauri wakaazi umuhimi wa kujiunga katika makundi ya vyama hasa wakati hitaji linapotokea
By Sajida Javan