Serikali imetakiwa kuingilia kati ya ugavi wa mashamba na wizi wa mahindi unaotekelezwa na waakazi wa Embambwa .
Katika mahojiano ya moja kwa moja na kurunzi ya 102.2 Lubao FM Joseph Machunja ambaye ni mzee wa kijiji cha Embambwa kata ndogo ya Sichirai kata ya Lurambi kaunti ya Kakamega amesema kuwa kesi zinazohusiana na ugavi wa mashamba baina ya wenyeji zimekithiri na kuwa kilio cha kila siku.
Joseph amesema kuwa huu ukiwa ni msimu wa mavuno shambani ametaja kuwa wizi wa mahindi umekuwa ni changamoto inayowakumba wakaazi.
Mzee wa kijiji ameiomba serikali kuingilia kati na kuwapa wenyeji usalama tosha.
By Mary Owano