Wakazi wa wadi ya Butsotso Mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wametahadharishwa dhidi ya matapeli ambao wananunua mbegu na mbolea ya kaunti na kuweka kwenye mifuko na kuwauzia wakazi kwa bei ghali

Akiwahutubia wombolezaji eneo la Emmachembe, afisa wa serikali ya kaunti ya Kakamega anayesimamia eneo la Shitoto Butsotso Mashariki Edward Obonyo amewataka wakazi kushirikiana na serikali kuwaanika wahusika huku akiwahimiza kutembelea afisi za kilimo kupata mbegu na  mbolea ya bei nafuu

Msimamizi wa shirika la kijamii la Jisimamie Community based organization katika wadi hiyo ya Butsotso mashariki Cyrus Akhonya amewahimiza wakazi kujitokeza na kuona kwamba wanashirikiana kuwapeleka watoto shuleni kupitia kwa mradi wa jisimamie elimu initiative

Story by Kefa Linda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE