Kauli ya kuwataka viongozi kuwa na kiwango cha shahada kwenye uchaguzi mkuu ujao imepigiwa upato na mbunge mteule kwenye bunge la kitaifa Godfrey Osotsi
Akizungumza na kituo kimoja cha radio kaunti ya Kakamega Osotsi ametaka pawepo viwango vya elimu hasa kwa wabunge kuwa na shahada ila akisema kwa wabunge wa kaunti akipendekeza wawe na kiwango cha diploma
Wakati uo huo Osotsi amesema miungano ya kisiasa inayobuniwa kwa sasa ya kisiasa haina nguvu mbele ya uchaguzi mkuu ujao.
Osotsi amepuzilia mbali makali ya muungano unaowaleta pamoja kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetang’ula na kiongozi wa chama cha KANU Gideon Moi wa One Kenya Alliance.
Osotsi amewashauri vigogo hao kumshawishi kinara wa chama cha ODM Raila Odinga au naibu wa Rais William Ruto kujiunga nao ili kupata makali ya kisiasa
Osotsi ametangaza azma ya kuwania kiti cha useneta kaunti ya Vihiga kwenye uchaguzi mkuu ujao kumridhi seneta wa sasa George Khaniri
By Javan Sajida