Viongozi mbalimbali kutoka eneo bunge la Mlima Elgon wameshauriwa kuhakikisha wanawapa msaada wa kutosha wakulima wa zao la kahawa ili kuwawezesha kunufaika kutokana na zao hilo.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi katika kijiji cha Kang’anga eneo bunge la Mlima Elgon, mwanaharakati wa kisiasa kutoka eneobunge la Mlima Elgon, Moss Ndiema amesema kilimo cha kahawa kimechangia pakubwa ukuaji wa uchumi wa eneo hilo na kuongeza kuwa ipo haja kwa viongozi kuingilia kati upesi  kuhakikisha wakulima wa kahawa wanapata kipato cha juu.

Aidha Ndiema amedai kuwa uongozi wa serikali ya kaunti ya Bungoma umetenga eneo bunge la Mlima Elgon kwenye maswala mbalimbali  akihoji kuwa nyingi ya miradi ya maendeleo haijatekelezwa kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE