Mkurugenzi wa shirika la utafiti wa kilimo Kalro kanda ya Magharibi Carolyn Kundu amewataka viongozi kuwasaidia wakulima kuendeleza kilimo cha kisasa

akiongea alipoongoza maafisa wa shirika hilo kuzuru baadhi ya mashamba ambako mbegu mpya ya mahindi imepandwa kwa majaribio maeneo ya Indangalasia na Lurambi na Ematiha ya Navakholo kaunti ya Kakamega amesema wanalenga kubaini mbegu itakayowapa wakulima faida

Amewahimiza wakulima kushirikiana na kituo hiki kupata mafunzo ya kilimo


Aidha bi Kundu amaewataka viongozi hasa wa kisiasa kushirikiana na Kalro kuona kwamba wanawafikia wakulima mashinani kubadili mbinu za kilimo

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE