Chifu wa Butsotso Mashariki kaunti ya Kakamega Justus Mukoshi amewataka vijana wanaotoka mashinani kutafuta ajira mijini kuwaelezea wazazi kuhusu maeneo yao ya kazi kuepuka sintofahamu
Akiwahutubia waombolezaji katika kijiji cha Emusala kwenye mazishi ya kijana Abraham Nambala ambaye alifariki katika hali tatatanishi baada ya kuondoka nyumbani mwezi Februari, Mukoshi amesema ni muhimu kwa wanafamilia kujua waliko wapendwa wao
Aidha chifu Mukoshi amewataka wakazi kuzingatia masharti ya kuthibiti corona na kujitokeza kwa chanjo wakati serikali itakapo tangaza bila kupotoshwa kuhusu madhara ya chanjo
Kwa upande wake naibu wa chifu wa kata ndogo hiyo ya Indangalasia Scholastica Jirongo amekashifu ongezeko la dhuluma za kijinsia
By Lindah Adhiambo