Wafanyakazi wa Chuo cha Moi wakiwemo wahadhiri na, wametishia kuandamana kwa kile wanasema kilio chao hakisikizwi na usimamizi wa Chuo hicho.

Wakiongea nje ya afisi kuu ya Chuo hicho zilizoko behewa la Kesses, wafanyakazi hao wamelalamikia masuala kadhaa ikiwemo ukosefu wa Bima ya Afya, kucheleweshwa kwa mishahara na marupurupu yao.

Kwa upande wake Naibu chansela wa Chuo hicho profesa Isaac Kosgei, amewarai wafanyikazi hao kuwa na subira wakati malalamishi yao yanashughulikiwa.

Ni malalamishi ambayo yalihusisha maslahi ya wanafunzi huku uongozi huo ukikiri kuna shida na unafanya kila juhudi kuimarisha hadhi ya Chuo hicho. 

Story by Alovi Joseph

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE