Akina mama Kaunti ya Bungoma wameshauriwa kujisajili katika vikundi na kupewa pesa za mikopo kutoka hazina ya akina mama ya Women Enterprise Fund ili kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumza wakati wa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita nukta sita kwa vikundi vya akina mama, Charles Mwirigi ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Hazina hiyo, amesema idadi ya vikundi vya akina mama vilivyosajiliwa katika Kaunti hiyo ni ndogo mno kufikia sasa.

Amesema Hazina hiyo inalenga kuongeza mgao wa fedha kuwafikia akina mama mashinani kama njia mojawapo ya kuwawezesha kiuchumi.

“Tumesikizana wakati tutarudi hapa vikundi vitakua vimeongezeka vya akina mama na tutapeana pesa ya 750 000 na wale ambao wako kwa 500,000 walipe haraka na wasonge vilevile hiki kikundi ni kama shule tunasonga polepole. Alisema  Mwirigi

Kwa upande wake mkewe gavana Kaunti ya Bungoma Bi Caro Wangamati amewataka akina mama walionufaika na mikopo hiyo kuitumia vyema ili kujistawisha kiuchumi.

Zaidi ya akina mama mia tano waliosajiliwa chini ya vikundi kutoka Kaunti ya Bungoma wamenufaika na fedha hizo za mikopo.

Story by Hillary Karungani

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE