Kwa Mara ya pili, wafanyakazi wa Chuo kikuu cha Moi wakiwemo wahadhiri wamesusia kazi kwa kile wamedai matakwa yao hayajashughulikiwa vikamilifu. 

Wakihutubia wanahabari nje ya ofisi Kuu ya Chuo hicho, wafanyakazi hao kupitia katibu mkuu wa Muungano wa wahadhiri wa Vyuo vikuu, UASU, Jack Willis, wamelalamikia Kutosikizwa na usimamizi wa Chuo hicho licha ya wao kutaka kuongea na uongozi wa Chuo hicho bila mafanikio. 

Kwa sasa, wafanyakazi hao wamerai usimamizi wa Chuo hicho kuchukuwa hatua na kuwasikiza huku wakitaja changamoto zao ikiwemo Kucheleweshwa kwa mishahara, ukosefu wa marupurupu na kutokuwepo kwa Bima ya Afya kwa wafanyikazi. 

Haya yanajiri wiki mbili baada ya wafanyikazi hao kutishia kuandamana wakilalamikia masuala hayo ila Naibu chansela wa Chuo hicho Isaac Kosgei akawaomba wawe watulivu wakati wanashughulikiwa.

Story by Alovi Joseph

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE