Uamzi wa kamati ya kilimo katika bunge la seneti wa kumtaka meneja mrasimu wa kampuni ya sukari ya Mumias kuweka wazi mchakato wa kukabidhi kiwanda hicho kwa mwekezaji wa kibinafsi umepongezwa na wakulima wa miwa eneo la Mumias
Wakulima hao sasa wanataka uwazi katika mchakato huo, wakiwarai wanasiasa kukoma kuingiza siasa katika maswala ya kiwanda hicho.
Wakiwahutubia wanahabari mjini Mumias, wakulima hao wameapa kumuunga mkono mwekezazi yeyote atakachaguliwa kwa njia ya uwazi wakidai hiyo ndio njia ya pekee ya kufufua uchumi wa eneo hili
Haya yote yanajiri baada ya madai kuibuka kuwa tayari kampuni ya sukari ya mumias ilikua imekabidhiwa kwa kampuni delvik, madai yaliyompelekea seneta wa kakamega kulitaka bunge la seneti kuingilia kati
By James Nadwa