Siku moja tu baada ya wakulima wa kahawa katika chama cha ushirika cha Chepkube eneobunge la Mlima Elgon kushiriki maandamano ya amani kulalamikia kile walichodai kunyimwa haki ya kushiriki zoezi la kuwachagua viongozi wao, sasa mkurugenzi wa vyama vya ushirika eneo hilo amejitokeza na kupuzilia mbali madai hayo na kusema sheria ilifwatwa kwenye mchakati huo.

Kwenye mkao na wanahabari mjini Cheptais mkurugenzi wa vyama vya ushirika eneobunge la Mlima Elgon Erick Kibet amepuzilia mbali lalama hizo akisema walifwata sheria wakati wa kuwapiga msasa wagombea viti mbalimbali kabla uchaguzi huo kundaliwa.

Aidha Kibet amedokeza kuwa hivi karibuni wataandaa mkutano maalamu ili kuwaelezea wakulima wa chama cha ushirika cha Chepkube kuhusu namna sheria  ilivyotumika kwenye uchaguzi huo.

Anasema wakulima wanaopinga uchaguzi huo hawana ufahamu kuhusu sheria za vyama vya ushirika.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE