Viongozi kutoka eneo bunge la Malava na eneo la Magharibi kwa ujumla wametakiwa kuungana pamoja na kuwaokoa wakulima wa zao la miwa kutokana na kunyanyaswa na viwanda vya kusaga miwa.

Wakiongozwa na aliyekuwa seneta wa Kakamega Bonny Khalwale viongozi hao wamezitaka kampuni za kusaga miwa za West Kenya na ile ya Butali kutii agizo la waziri wa kilimo nchini la kuwalipa wakulima kiwango cha pesa kisichopungua shilingi elfu nne na arobaini kwa kila tani ya miwa.

Wakizungumza kwenye hafla ya mazishi ya mzee David  Musungu Taliti katika kijiji cha Musungu, viongozi hao aidha wamezitaka kampuni hizo kukoma kuwadhulumu wakulima wa miwa la sivyo hawatakuwa na budi kuandaa maandamano katika juhudi za kukomesha dhulma hiyo.

Ikumbukwe kuwa hivi maajuzi waziri wa kilimo Peter Munya aliziamuru kampuni za kusaga miwa kuwalipa wakulima shilingi elfu nne na arobaini kwa kila tani  amri iliyopaswa kuanza kutekelezwa kutoka tarehe mosi mwezi huu wa nne.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE