Washirika wa kanisa la PAG Makutano ilioko Mungulu wadi ya Butsotso Mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wamepigwa na butwaa walipofika kanisani na kupata nyumba ya mchungaji imevunjwa na watu wasiojulikana na kuiba

Nyumba hiyo ya mchungaji wa kanisa hili anayejulikana kama pastor Wycliffe Sajida ilibomolewa usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe kumi na saba na kuiba mali ikiwemo gas cooker, extension ya Umeme, nguo za mchungaji, viatu, vitambaa vya kanisa bila kuwacha vyakula vilivyokua ndani ya kabati na kusema kua kisa hiki si cha kwanza.   

Waumini walijawa na hasira kwa sababu ya hicho kitendo huku wakikilaani vikali na kutaka serikali kuingilia kati na uchunguzi kuanza ili kunasa waliohusika na wizi wa vitu vya kanisa  

  Mmoja wa washiriki anayejulikana kama Ronnie alikashifu vitendo vya wizi nakusema kuwa mwezi uliopita naye pia aliibiwa kwenye duka lake vitu vyenye dhamana K. V televisheni na vyakula na kumwacha bila chochote hivyo basi kuitaka serikali iendelee na uchunguzi na kuweka ulinzi kwenye mitaa.   

 Kiongozi wa nyumba kumi Elukaka Joseph ameonya kwamba atakaye one kana usiku na kuonekana mwenye nia mbaya atapewa adhabu kali na kutaka OCPD, OCS na chifu wasaidie wanapo shika watu ili wasirudi tena na kuendeleza maovu.                                                                                         

Kwingineko mzee wa mtaa alikua na usemi kwa wazazi kuwa wachunguze watoto wao na kujua hasaa vitu ambavyo wanajishugulisha navyo ili kupunguza visa vingine vibaya

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE