Wenyeji wa kijiji cha Muranda eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega walishikwa na butwaa baada ya washukiwa wawili  wa wizi  wa ngurwe akiwemo Alexander Musava na Nicholas Inganji  kukula nyasi  kama mnyama.

Kulingana na wenyeji wakiongozwa na Edgar Muhanga wanadai kuwa wawili hao walimuibia mama Dorice Achitsa  nguruwe wawili na walipoulizwa wakakana jambo lilopelekea kutafuta usaidizi wa mganga kutoka kaunti ya Busia ambaye alifanya nganga nganga zake na kupelekea wawili hao kula nyasi.

Mwenye boma hilo Dorice Atsitsa anasema kuwa mara nyingi amekuwa akipoteza mali ya maelefu ya pesa hasa nyakati za usiku.

Ilibidi familia ya wawili hao pamoja na mlalamishi kumuita daktari huyo Okello ambaye alifika na kuwanasua washukiwa hao ambao walikuwa wakiendelea kukula nyasi  huku  akiwaonya walio na tabia sawia na hiyo.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE