Wazazi na washikadau kutoka sekta mbalimbali wamehimizwa kuingilia kati na kuwapa watoto mafunzo ya ziada hasa wale wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza ili kuwaepusha kujiingiza kwenye visa vya maadili potovu.

Akihutubu baada ya kuhudhuria ibaada ya jumapili katika kanisa la katoliki la Our Lady  Queen of Peace Cheptais eneobunge la Mlima Elgon padre wa parokia hiyo Protus Osianju anasema tayari kanisa hilo limeanzisha mpango wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi  wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza akiwataka washikadau wengine kuunga mkono mpango huo.

Wakati uo huo Padri Osianju amewataka wananchi kufwata maagizo ya wizara ya afya ili kujizuia dhidi ya maambukizi ya homa ya corona.

Anasema kuanzishwa kwa parokia ya Cheptais tayari kumechangia kuwepo uwiano na amani miongoni mwa jamii zinazoishi eneobunge la Mlima Elgon.

By Ricahrd Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE