Wakulima wengi eneo la Magharibi wanaendelea kutayarisha mashamba yao tayari kuendelea na shughuli za upanzi wa mimea na vyakula tofauti shambani.

Licha ya kuwepo kwa kiangazi kirefu msimu huu wakulima bado wanaendeleza kuyaweka sawa mashamba yao ingawa wengine wanahofia madhara ya kiangazi kwa shughuli zao za upanzi.

“Majina yangu ni koko au mama Regina Mrombotho mwaka Jana mvua ilikua karibu kwa sababu nilipanda mwezi wa pili tarehe mbili na leo naona mvua iko mbali na nimeona hapa panakauka na ndio nimeona nieke mbegu chini nisichelewe kupanda.”

Msimu huu kiangazi kimekuwepo kwa muda mrefu ikilinganishwa na mwaka Jana ambapo wakati Kama huu wengi wa wakulima walikuwa tayari wamepanda mimiea yao hasa mahindi.

Shughuli za upanzi wa vyakula tofauti kwa wakulima huwa ni miradi inayohitaji kujiandaa kwa njia iliyobora ili kupata mavuno na manufaa baadae.

“Kwa majina ni Ebby Khasandi,mimi ni mkulima wa ACRE FUND,tumeona tupande mahindi lakini ingawa mvua ingali mbali,tunaona tupande mvua ipate mahindi chini juu ikinyesha mahindi itatoka ikiwa na nguvu sana”.Mkulima mmoja aliongezea.

By Austine shambetsa.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE