Walimu wakuu wametakiwa kuwa waaminifu pamoja na kudumisha ushirikiano baina yao na bodi simamizi za shule katika kutekeleza miradi ya shule.

Haya ni kwa mujibu wa aliyekuwa mwalimu mkuu mstaafu wa shule ya upili ya wavulana ya  Kimang’eti iliyoko eneo bunge la Malava Masai Mwalati ambaye anahoji kuwa walimu wakuu wanapaswa kuwajibika ipasavyo na kuwahusisha wadau husika katika kuendesha mipangilio ya shule.

Kwa upande wake mwakilishi wa kijinsia katika chama cha KUPPET tawi la Kakamega Leah Khasandi akiwataka wananchi kufanya uamuzi ulio bora katika kuwachagua viongozi wa kisiasa  na wala siyo kwa  mapendeleo ya kikabila.

Wawili hao walikuwa wakizungumza kwenye hafla ya sherehe ya kustaafu kwake mwalimu Masai Mwalati katika kijiji cha Shitirira ambaye amehudumu kama mwalimu kwa zaidi ya miaka 30. 

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE