Vijana katika eneo la Khwisero kaunti ya Kakamega wameitaka serikali kupata mbinu mbadala ya kuwasaidia kupata vifaa vya kuwazuia na maambukizi ya corona badala ya kuwashika na kuwashitaki kila wakati hasa kwa kukosa barakoa
Wakiongozwa na Rashid Inganga Mbaye alijitokeza kuwapa wakazi wa wadi ya Kisa Kaskazini barakoa na sabuni wamesema idadi kubwa ya vijana na akina mama wanakamatwa na kutozwa faini ila hali mapato yao yamekuwa magumu kutokana na janga la corona
Baadhi ya wakazi wa kisa kaskazini ambao walinufaika na usaidizi huo walisema wamepata afueni
By Imelda Lihavi