Mwenyekiti wa shirika la wakulima la Kenya National Federation of Farmers tawi la kaunti ya Kakamega Habbakuk Khamala ameitaka serikali ya kaunti kushauriana na wakulima na kujua mahitaji yao kabla ya kutekeleza ununuzi wa pembejeo kuhakikisha zinawafaidi wakulima
Akiongea alipoongoza afisi ya KENAFF kutembelea vikundi vilivyo chini ya shirika hilo katika wadi ya Butsotso Mashariki chini ya kundi la Jisimamie CBO Khamala amesema inasikitisha serikali kununua vifaa ambavyo havitumiki na wakulima
Vile vile Khamala amesema wanaendelea na mradi wa upanzi wa miti huku akiwahimiza wakulima kujiunga kwa vikundi kuweza kufikiwa kwa haraka na serikali na mashirika
By Richard Milimu