Mwakilishiwadi wa Marama Central kaunti ndongo ya Butere Ondako Maina amewakashifu wapinzani wake kisiasa kwa kutumia swala la barabara kujitaftia umaarufu kisiasa
Ondako amehusisha Hali hiyo na kucheleweshwa kwa hela kutoka kwa serikali kuu kuja kwa zile za kaunti kwa kuathiri maendeleo mashinani haswa miundomsingi
Amewataka wapinzani wake kumpa nafasi kuwatekelezea wakaazi ahadi alizowapa wakati wa kampeni
Ondako ametaja baadhi ya barbara alizozokamilisha licha ya changamoto hiyo
Licha ya kutumia fedha za kustawisha maendeleo kwenye Wadi Ondako vilevile amesema kuwa atashirikiana na mashirika mbalimbali kuwasaidia wanafanunzi kutoka jamii zisizojiweza walopita mtiani kuendelea na masomo yao
By James Nadwa