Jumla ya wanafunzi 236 katika Kaunti ya Bungoma wamenufaika n ufadhili wa elimu chini ya mpango wa Wings to Fly na Elimu program unaofadhiliwa na Benki ya Equity na Benki ya Dunia 

Kwa mujibu wa Meneja wa Benki ya Equity Tawi la Bungoma Stephen Wasiche, amesema mpango wa kuwachagua watakaonufaika umekuwa wazi kwa kuzingatia wanafunzi bora kutoka familia maskini Kaunti ya Bungoma

Wasiche aidha amesema mbali na kutoa ufadhili huo wa elimu, Benki ya Equity pia inatoa uhamasisho kwa wanafunzi walionufaika ili kuepusha visa vya utovu wa nidhamu wakiwa shuleni.

Ni hafla iliyohudhuriwa na waziri wa elimu Kaunti ya Bungoma Dakt Betty Mayeku, akiipongeza Benki ya Equity na washikadau wengine kwa kufadhili elimu.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE