Wito umetolewa kwa serikali za  kaunti nchini kukumbatia mfumo wa ufadhili wa elimu almaarufu kama scholarship kwa wanafunzi badala mfumo wa sasa wa CDF bursary  kwa wanafunzi

Hayayamesemwa na mkurugenzi mkuu benki ya Equity nchini James Mwangi wakati wa hafla iliyowaleta pamoja wanafunzi zaidi ya mia tano wanaojiunga na shule za upili mwaka huu kutoka kaunti ya Busia walionufaika na mpango wa Wings to Fly kwa ushirikiano na wakfu wa elimu -Elimu Scholarship Program nchini.

 Mkurugenzi  huyo aidha ameusuta mfumo wa sasa unaotumika katika maeneo bunge almarufu [bursary] huku akisema kuwa wengi wa wanafunzi wanaopata ufadhili huo hupata chini ya shilingi  elfu mbili fedha ambazo amesema ni chache mno kukidhi mahitaji ya mwanafunzi.

By Hilary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE