Ni afueni kwa wanafunzi  mia sita sabini kutoka ukanda wa magharibi  wanaosemekana kunufaika na benki ya Equity kuendeleza masomo yao ya kidato cha kwanza baada ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo James Mwangi kutoa  barua za udhamini kwa wanafunzi hao kutokana na matokea mema waliyoweza kupata kwenye mtihani wa darasa la nane uliopita .

Changamoto ikiwa kwa wale ambao wanatarajia kukalia mwaka huu ili nao pia kupata ufadhili huo.

Akiongea shule ya upili ya Kakamega alipokutana na wanafunzi hao ili kuwapa barua hizo za ufadhili mkurugenzi huyo amempongeza rais Uhuru Kenyatta kutokana na ushirikiano wa karibuu na washikadau kwenye benki hiyo  jambo ambalo amesema kuwa baadhi ya sababu ambazo zimechangia ufadhili wa wanafunzi wengi wasiojiweza nchini.

Wakati huo mkurugenzi huyo amewashauri walimu  ambao watapokea wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanaendeleza bidii kwa wanafunzi hao ili wanajiunga na vyuo mbalimbali nchini

Ni matamshi ambayo yameungwa mkono na naibu gavana wa kaunti ya Kakamega  Philip Kutima ambaye  amewataka wanafunzi hao kutia bidii kwenye masomo yao ili kuwa daraja la uvukio kutoka  lindi la umaskini ambalo linasemekana kuzingira wengi nchini

Kando na kauli hiyo kushahabikiwa na wengi akiwemo  chifu wa Sheywe baadhi ya walimu wamemtaka waziri wa masomo nchini kuachilia kuwepo kwa shule za bweni ili kusaidia wanafunzi kupatikana kwa haraka wanapohitajika na walimu

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE