Wizara ya afya Kaunti ya Bungoma kwa ushirikiano na wizara ya afya katika serikali ya Kitaifa zinanuia kuanzisha mpango wa kuwapa dawa za minyoo wanafunzi wapatao 600,000 katika Kaunti ya Bungoma kama njia mojawapo ya kuwasaidia wanafunzi kutosumbuliwa na minyoo.
Haya yamethibitishwa na Dakt Antony Walela waziri wa afya katika serikali ya Kaunti ya Bungoma akiwa katika mkutano uliowaleta pamoja washika dau wa elimu na afya kutoka serikali ya kitaifa na ya Kaunti, mkutano ulioandaliwa katika taasisi ya mafunzo ya ualimu ya Kibabii diploma teachers college.
“Watu wengi watasema watoto hawana minyoo lakini aslimia sabini ya watoto wana minyoo. Dawa hizi tutawapatia watoto na zingine tutawapa wale wahudumu wa afya wa kujitolea vijijini.” Alisema Dakt Antony Walela