Ni afueni kubwa kwa wanafunzi wa shule ya upili ya Mtakatifu Monica Lubao baada ya wanafunzi 100 kufaidika na mradi wa Baiskeli aina ya Bufallo kutoka kwa shirika la kibafsi la World Bicycle relief ambalo limewapokeza baiskeli hizo ikiwa ni mara ya pili baada ya kupokezwa mara ya kwanza mwaka wa 2019

Akizungumza na kituo hiki msimamizi wa shirika hilo kitengo cha elimu Peter Wechuli amesema mradi huo utawasaidia pakubwa wanafunzi katika kuinua viwango vyao vya elimu kiujumla huku akiipongeza idara ya elimu kaunti ya Kakamega kwa kushirikiana nao vyema kwenye mradi huo.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Peter Echesa amepongeza shirika hilo kwa kujali pakubwa shule hiyo akisema mpango huo utawapa wanafunzi motisha katika kuimarisha viwango vyao vya masomo

Kauli iliyopigwa jeki na naibu chifu wa kata ndogo ya Lubao Sulvei shiafu ambaye ameushabikia msaada huo anaoamini utawafaidi pakubwa wanafunzi wa shule hiyo.

Kwa upande wao wazazi wa shule hiyo pia wameshabikia mradi huo wakisema umewaondolea mzigo mkubwa wa kulipia nauli ya wanao kwenda shuleni.

Story by Sajida Javan

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE