Biwi la simanzi lingali limeigubika familia moja kutoka kijiji cha Mungakha wadi ya Namamali eneobunge la Matungu kaunti ya Kakamega baada ya mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi ya Mungakha kujitia kitanzi mapema leo asubuhi na kuaga dunia….
Kulingana na wazazi wa mtoto huyo ni kwamba mwanao mwenye umri wa miaka kumi na sita amewaelezea kuwa amekuwa akifwata na mapepo yaliyomkosesha amani jambo lililopania yeye kujitia kitanzi………….
Aidha familia hiyo inasema ni pigo kubwa kwao kwani mwanao alikuwa mtahiniwa wa darasa la nane mwaka huu kando na kuwa mtoto wa bidii na mwenye nidhamu.
Story by James Shitemi