LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

Wezi kula nyasi Westkenya eneobunge la Malava Kaunti ya Kakamega

Wenyeji wa kijiji cha Westkenya eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wamejionea kioja baada ya watu wawili ambao ni wahudumu wa baa moja eneo hilo kugeuka kuwa wazimu kufuatia madai ya kushiriki wizi eneo hilo.

Wawili hao ambao ni mwanamme mwenye umri wa miaka 36 na mwenzake wa kike wa miaka 27 wakiwa wafanyikazi wa eneo moja la burudani wanadaiwa kushiriki wizi wa zaidi ya shilingi elfu thelathini na tano, vifaa vya elektroniki pamoja na pombe baada yao kunaswa na daktari wa miti shamba anayedaiwa kutoka kaunti ya Busia.

Ni tukio lililowaacha wakazi wa eneo hilo wakiwemo wafanyibiashara mbalimbali na mshangao mkubwa wakisema visa vya wizi vimekithiri pakubwa katika eneo hilo huku wakiwataka wakazi kujituma kufanya kazi badala ya kushiriki visa vya wizi.

Story by Sajida javan

sadmin

Read Previous

Wanafunzi kupokezwa baiskeli katika shule ya upili ya Mtakatifu Monica Lubao

Read Next

Kenya National Qualificationa Authority Kuanzisha mpango wa kupiga marufuku vyeti gushi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *