Baraza la wahariri limeanzisha mpango wa utoaji mafunzo kwa wanahabari katika bara la afrika yakijumuisha jinsi watakavyojikinga dhidi ya virusi vya korona hasa wakati huu ambapo mataifa yanashuhudia wimbi la tatu la maambukizi.

Rais wa baraza hilo churchill otieno, katika tarifa yake anasema mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha wanahabari wanapata taarifa muhimu na sahihi kuhusu ugonjwa wa covid-19.

Otieno anadokeza kwamba mafunzo hayo yatatolewa kwa ushirikiano na shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni unesco huku mafunzo hayo yakitolewa kati ya tarehe 14, 15, 16 hadi 19 mwezi aprili kuanzia saa mbili saa za afrika mashariki.

By Austin Shambetsa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE