Maafisa wa polisi eneo bunge la Khwisero kaunti ya Kakamega wamefanikiwa kunasa washukiwa wawili wa ubakaji huku pia wakitazamiwa kuwanasa watahiniwa watatu wanaodaiwa kuwabaka wanafunzi wa shule ya upili ya Mundoli.
Wawili hao wanadaiwa kuwabaka mama na wanawe wawili mtawalia katika kijiji cha Khumusalaba nyakati za usiku, huku mama mwathiriwa Gedray Majunga Ukom akieleza kuwa washukiwa watatu wakiwa wamejihama kwa silaha butu walibomoa mlango na kuingia kisha kuwaamrisha kuvua nguo zote kisha kuwatendea unyama huo.
OCPD wa Khwisero Samwel Kogo amethibitisha kukamatwa kwa wawili hao,na kusema vilevile maafisa wa polisi wanalenga kuwatia mbaroni washukiwa wa ubakaji ambao ni watahiniwa wa kidato cha nne kwa tuhma za kuwabaka wanafunzi watatu wa shule ya upili ya Mundoli.
By Linda Adhiambo