Mwakilishiwadi wa Marama Central gatuzi dogo la Butere Ondako Maina amesema kuwa sharti wakaazi wapewe mafunzo ya kutosha kuhusu BBI kabla ya kuandaliwa kwa kura ya maoni
Kwenye kikao na wanahabari Ondako hata hivyo amehoji kuwa yafaa vyongozi haswa wa mashinani kuhusishwa kwenye uhamasisho huo
Mwakilishiwadi huyo hata hivyo ameunga mkono pendekezo la wanasiasa kuwa na kiwango cha degree kwenye masomo yao ndiposa waruhusiwe kuwania kiti cha uakilishiwadi
Kiongozi huyo aidha ameusuta mrengo wa tangatanga kwa kuupotosha umaa kuhusu BBI
Story by James Nandwa.