Kiranja wa wengi katika bunge la kitaifa ambaye pia ni mbunge wa Navakholo Emmanuel Wangwe amelitaka jopo la sukari kuwasilisha ripoti yake Bungeni ili kujadili na mapendekezo yake idhinishwe kufufua viwanda vya sukari vilivyokwama eneo la magahribi .

Akihutubia waombolezaji katika kijiji cha  Buhayi kwenye mazishi ya Agrrey Musii mumewe Lilian Musii chifu wa kata ya Bunyala Mashariki  Wangwe amehoji kuwa licha ya ripoti ya jopo hilo kuwasilishwa kwa rais, imecheleweshwa kufikishwa bungeni hivyo  kusitisha juhudi zote za ufufuzi wa viwanda kikiwemo cha mumias..

Mwakilishi wa wadi ya Shinoyi/ Shikomari/ Esumeyia ambaye pia ni kiranja wa wengi katika bunge la kaunti ya Kakamega Boniface Akosi amedai kama jamii ya mulembe watawaunga tu mkono viongozi waliotatua tatizo la ukuzaji wa miwa ikizingatiwa kuwa ndicho kitega uchumi eneo hilo.

Akosi ametokeza kuwa kwa sasa wakulima wa miwa wanapitia changamoto nyingi kuvuna miwa yao kwa kukosa kupata vibali vya kuvuna mazao yao kutoka kwa viwanda vya kusiaga sukari.

Wangwe aidha amewasuta viongozi wanaokashifu azma ya kinara wa chama cha anc muasalia mudavadi kuwania urais mwaka 2022 kuwa wenye ubinafsi unaokandamiza umoja wa jamii ya magaharibi

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE