Kwa mara nyingine mjumbe wa Kiminini daktari Chris Wamalwa ametoa wito kwa rais kuyaruhusu maeneo ya kuabudu kuendelea kufanya kazi,
Akizungumza mda mchache na wanahabari baada ya kuwasili nyumbani kwake ,dkt Wamalwa amelisikitikia swala la waumini kusalia nyumbani siku za ibada huku shughli zingine zikiiendelea huku akisema kuwa ni ibada pekee itakayoikomboa taifa kutokana na Janga la korona,
Mjumbe huyo aidha ametilia hofu kwamba huenda visa vya upotovu wa nidhamu haswaa miongoni mwa vijana vikapanda juu kutokana na wao kukosa kupata ushauri wa kidini,
Hivyo basi daktari Wamalwa amemuomba rais Uhuru Kenyatta kuubadili msimamo wake wa hapo awali wa kuyafunga maeneo ya kuwabudu kwa mda na kuwaruhusu wauminui kuendelea na ibada kama ada,
Usemi wa mjumbe huyo unakujia siku moja tu baada ya usemi sawia na huo kutoka kwa askofu wa kanisa la ki Anglikana Philip Mechumo.
By Hillary Karungani