Akiongea eneo la Shiamoni kwenye mazishi ya mama Rose Wayiera Malulu amesema tayari usimamizi bora wa CDF chini ya uongozi wake umeimarisha masomo na kwa sasa zaidi ya wanafunzi mia nne wanapata alama za kuwapeleka vyuo vikuu
Malulu amewataka walimu kutowalipisha wazazi ada za ujenzi akisema hazina ya CDF imewajikia jukumu la kuinua miundo msingi kwa shule
Mwakilishi wadi ya Kabbras Magharibi David Ndakwa amewataka wazazi kuwa macho na wanawao hasa wakati huu wa likizo na kuwataka machifu kuwachukulia hatua wale watakaopatikana wakiwadhulu wanafunzi kimapenzi
Kwa upande wake naibu chifu wa Shiamoni Vitalis Otisa amewataka wakazi kuzingatia maagizo ya afya na kujikinga dhidi ya maambukizo ya corona