Hali ya huzuni imetanda maeneo ya Stendi Mwogo wadi ya Butsotso ya kati eneo

Bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega baada ya mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi ya Elwaminyi darasa la tano kufariki papo hapo na mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo akijeruhiwa vibaya baada ya pikipiki waliokuwa nayo kuingia nyuma ya gari ndogo liliyokuwa mbele yao kwenye barabara kuu ya Kakamega kuelekea maeneo ya Mumias jana jioni.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa marehemu ambaye ni mwanadamu wa darasa la tano alikuwa amewabeba wanafunzi wenzake wawili kwenye pikipiki hiyo akiendesha kwa njia ya kasi wakitoka upande wa Kakamega na walipofika maeneo ya Stendi Mwogo waligonga gari ndogo aina ya probox lililokuwa mbele yao kabla ya gari lingine lilokuwa likitoka upande wa pili  kuwakanyaga  huku aliyekuwa akiendesha pikipiki hiyo akifariki papo hapo.

Aidha wenyeji wa sehemu hiyo wakiwemo wahudumu wa bodaboda wamelalamikia ajali nyingi kutokea sehemu hiyo huku watu wengi wakipoteza maisha na kutaka idara husika kuweka matuta kwenye barabara hiyo la sivyo waandamane na kuweka matuta kuzuia ajali za mara kwa mara.

Mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali kuu ya kaunti ya Kakamega huku aliyejeruhiwa akiendeleza kupata matibabu kwenye hospitali hiyo.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE