Wazazi wamehimizwa kuwapeleka wanao shuleni ili kupata haki ya Elimu kwa kila mtoto.
Ni kauli yake mwakilishi wadi ya Kabras Magharibi David Ndakwa akihutubia waombolezaji kwenye ibada ya mazishi ya mama Florence Charles Kakai kwenye eneo Bunge la Malava Kaunti ya Kakamega
Ndakwa amewarai pia wakaazi wa Malava kuwapiga msasa vyema viongozi wote kabla ya kufanya uamuzi kwenye uchaguzi mkuu ujao
Naye mwakilishi wadi ya Kabras Kusini Samson Serengo Tali akiwataka wazazi kwenye eneo bunge la Malava kutumia chuo cha mafunzo cha Shamberere na kuwapeleka wanao kujifunzia taluuma mbalimbali.
Wakati uo huo Tali amewataka wakuu wa kampuni ya kiwanda cha kusaga miwa cha West Kenya kujukumika na kusaidia maendeleo kwenye eneo bunge hilo ikiwemo Kukarabati baadhi ya barabara ambazo hutumikiwa na trakta za kampuni hiyo
By Ernest Luvisia

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE