Maafisa wa polisi walilazimika kutumia vitoa machozi kutawanya kundi la wahudumu wa bodaboda pamoja na wanafunzi wa chuo cha anuai cha Shamberere waaliokua wakiandamana na kufunga barabara ya Kambi ya Mwanza kuelekea Lukume wakilalamikia hali mbovu ya barabara hiyo.
Wakizungumza na kituo hiki kwenye barabara hiyo wahudumu hao wamedai kuwa usimamizi wa kiwanda cha sukari cha West Kenya umekua ukitoa ahadi hewa kuhusu kukarabati kwa barabara hiyo kabla yao kuandamana na kulemaza shughuli nyingi eneo hilo
Kwa upande wao wanafunzi wa chuo chs Anuai cha Shamberere ambao pia walishiriki maandamano hayo wamelalamikia ukosefu wa taa karibu na Chuo hicho wakihofia usalama wao nyakati za usiku
Baadhi ya wakulima nao wameilaumu serikali ya kaunti ya Kakamega kwa madai ya kukosa kutumia vyema fedha wanazokatwa wakulima wa miwa maruufu kama CESS
Hata hivyo afisa wa mawasiliano kutoka kiwanda cha sukari cha West Kenya Edwin Musonye amesema kama kampuni wamekuwa wakikarabati barabara nyingi eneo hilo akiilaumu serikali ya kaunti ya Kakamega kwa kukosa kuajibikia swala hilo kwa muda mrefu sasa.
By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE